MATUKIO KATIKA PICHA, MAONESHO YA NANE NANE KATIKA VIWANJA WA JOHN MWAKANGALE JIJINI MBEYA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, August 2, 2017

MATUKIO KATIKA PICHA, MAONESHO YA NANE NANE KATIKA VIWANJA WA JOHN MWAKANGALE JIJINI MBEYA


 wafanya kazi wa kituo cha Radio cha Rock FM ya jijini Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na mwandishi wa Blog hii ya Mzalendo bwana  Sebastian Emmanuel jr mwenye fulana Nyekundu

 wakulima na wafanya kazi wa Sagcot pamoja na mdau wa kilimo bwana Emmauel Mwakabana mwenye flana ya punda milia wakionesha viazi mviringo ambavyo vinazarishwa na kampuni hiyo.


 Bwana Emmanuel Mwakanama afisa kilimo wa kampuni ya Syngenta akiwa kwenye Banda lao la maoenesho hayo.
 Ndivyo tulivyo karibishwa katika viwanja vya maonesho ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

 Wilaya ya Iringa nao hawapo nyuma katika maonesho hayo na tumeshuhudia wakionesha eneo hasa la utalii unao patika mkoa wa Iringa Mji Njombe nao wapo hapa Mbeya Nane Nane.
 Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi bwana Mpokigwa mwenye Flana nyekundu akisaini kitabu cha wageni alipo ingia kujifunza juu ya utengenezaji wa bidhaa ya maziwa kutoka Njombe Milk Factory
 Bwana Hongori Meneja mauzo wa Kiwanda cha Njombe Milk Factory akionesha bidhaa ya maziwa inayo uzwa kwenye maonesho hayo.

 Tigo nao wapo hapa tumewakuta wakiandaa sehemu yao
 wananchi katika maonesho hayo
 Na Sebastian Emmanuel jr.
Wananchi mbali mbali katka jiji la Mbeya na mikoa mingine inayo shiriki katika maonesho ya wakulima maarufu kama maonesho ya nane nane, wameendelea kujitokeza katika maonesho hayo kwa wingi huku wakiwa na shauku ya kutaka kuona vitu tofauti tofauti vya wajasilia mali pamoja na shughuli za kilimo kutoka katika wilaya mbali mbali.
Baadhi ya mabanda tuliyo yapitia ni Pamoja na Synigenta, Sagcot, banda la Wilaya ya Mufindi ambapo tumekutana na wajasilia mali mbali mbali pamoja na bidhaa zao, Banda la Halmashauri ya Iringa, Halmashauri ya mji Njombe pamoja na baadhi ya wajasilia mali na vituo vya Radio kadhaa vilivyo jitokeza kwenye maonesho haya.
Sisi Mwana harakati Mzalendo tumeweka kambi hapa katika viwanja hivi vya maonesho na camera yetu imepitia katika baadhi ya mabanda na kushuhudia shughuli mbalimbali za kijasilia mali zikiendelea. lakini kubwa zaidi ambalo tumeligundua hapa ni vyombo vya habari kuto yapa kipaumbele zaidi maonesho haya. ndio maana sisi Mwana harakati Mzalendo tumeamua kukaa hapa mpaka maoenesho yatakapo kwisha lengo ni kukuletea msomaji kila kinacho endelea hapa mpaka siku ya ufungaji wa maonesho haya ambapo Makamo wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Samia Suruhu Hassaniatakujua kutamatisha maonesho haya.

Loading...

No comments: