Mpinzani Mkuu wa Lungu atoka jela - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, August 17, 2017

Mpinzani Mkuu wa Lungu atoka jela

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zambia, Hakainde Hichilema aliyekuwa amewekwa mahabusu akikabiliwa na shtaka la uhaini ameachiliwa huru asubuhi hii.

Hichilema ameachiwa huru baada ya Mwendesha Mashtaka kumfutia mashtaka kiongozi huyo aliyekuwa mahabusu tangu Aprili mwaka huu.

"Mwendesha Mashtaka Mkuu ameamua kusitisha mchakato wa kesi kwa mamlaka ya kikatiba aliyonayo. Kwa hiyo, anaachiwa huru kuanzia sasa,” amesema Jaji wa Mahakama Kuu, Charles Chanda.

Hichilema na wenzake walikamatwa kwa madai ya kutaka kuhatarisha maisha ya Rais Edgar Lungu baada ya kiongozi huyo na wafuasi wake kukataa kupisha msafara wa rais huyo.

Habari za kuachiwa huru zilivuja tangu mwishoni mwa wiki, ikielezwa kwamba ni kutokana na juhudi zilizofanywa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland ambaye alifanya ziara nchini Zambia kuangalia hali ya siasa. Katibu huyo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Lungu na pia alimtembelea Hichilema katika gereza la Mukobeko.
Loading...

No comments: