Rais Magufuli Amuahid Cheo Kikubwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, August 4, 2017

Rais Magufuli Amuahid Cheo Kikubwa Mkuu wa Wilaya ya KorogweSeeBaitRais John Magufuli ameahidi hadharani kumpatia nafasi ya juu kati ya zile atakazokuwa nazo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhandisi Robart Gabriel kwa madai kuwa ni kiongozi anayejitoa kwa kufanya  kazi bora zinazoonekana katika wilaya yake.
Rais ametoa ahadi hiyo  jana  akiwa barabarani Hale Tanga kwenye ziara yake mkoani humo baada ya kusimama kuzungumza na wananchi waliosimama kumpokea ndani ya mkoa huo.
Mh. Magufuli alisema kazi anazofanya Mhandisi Gabriel ni za kuigwa kwani shughuli za maendeleo anazozitekeleza ni kubwa kuliko hata bajeti anayopatiwa hivyo ni jambo jema kwa kiongozi kutumia bajeti vizuri.
"Mkuu wa wilaya ya hapa anafanya kazi sana, ni kiongozi ambaye anatekeleza miradi mingi kwa wakati na ubora. Ameanzisha vikundi vidogo vidogo vinavyomsaidia kukamilisha miradi yake kwa usahihi lakini pia amejenga vyumba vya madarasa vingi kuliko pesa ya serikali iliyotolewa......Nakuahidi zile nafasi zangu za juu kama bado zipo lazima nikupatie kwani unanifurahisha sana"  alisema Rais Magufuli na kuongeza;
"Unajua watanzania mmezoea kuwasifu watu wakishakufa, kuwa pengo lake halitazibika kumbe mnaziba siku hiyo hiyo. Mimi namsifia kabla hajafa. nawaahidi mkuu wenu wa wilaya nitampatia nafasi na kwa vile hata mkuu wako wa kazi amenipa ripoti nzuri kuhusu wewe hivyo sina mashaka na wewe labda ubadilike leo baada ya kukusifia.....Wanakorogwe sifa za kiongozi wenu ni zenu pia kwahiyo nawapongeza." alisema Rais Magufuli
Loading...

No comments: