Serikali Yawapa Siku 7 Wakimbizi wa Burundi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, August 25, 2017

Serikali Yawapa Siku 7 Wakimbizi wa Burundi

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba, ametoa siku saba kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kuhakikisha linaanza zoezi la kuwarejesha Burundi wakimbizi walio tayari kurejea nchini  kwao.

Waziri Nchemba ametoa agizo hilo leo Alhamisi Agosti 24, baada ya kutembelea kambi za Nduta Wilaya ya Kibondo na Mtendeli wilayani Kakonko katika ziara maalumu.

Nchemba amesema iwapo siku saba zitafika kabla ya kuanza kwa zoezi hilo, serikali itatumia magari ya jeshi kuwarejesha kwao kwakuwa wamekubal wenyewe.

Kwa mujibu wa mratibu wa wakimbizi kanda ya Kigoma, Tony Laizer amesema hadi sasa Kambi ya Nduta imesajili wakimbizi 8,743 ambao wameridhia kurejea nchini kwao kwa hiari.

Mkuu wa makazi katika kambi ya Nduta, Peter Bulugu, amesema hali ya usalama si shwari maeneo ya kambi na nje ya kambi kutokana na baadhi ya wakimbizi kujihusisha na wizi na uvamizi unaotokana na ukosefu wa chakula cha kutosha na kushinikiza kurejeshwa kwao.

Kwa upande wa Mwakilishi wa shirika hilo ofisi ndogo wilayani kibondo, Barb Wigley ameiomba serikali kuwavumilia UNHCR kwakuwa vikao baina ya pande tatu yaani serikali ya Tanzania, Burundi na UHNCR vinaendelea ili kuwarejesha watu hao kwa staha.

Nchemba amesema msimamo wa serikali ni kuanza kuwarejesha wakimbizi hao katika muda uliopangwa.

Loading...

No comments: