Tigo watiliana saini na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, August 21, 2017

Tigo watiliana saini na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF)

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akitia saini ya Mkataba wa Kufikisha Mawasiliano Vijijini na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.  Wanaoshuhudia (katikati) ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na  Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa pamoja na maafisa wengine wa mfuko huo. Hafla hiyo ilishirikisha makampuni ya simu nchini. 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akipeana mkono wa pongezi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga mara baada ya kusaini mkataba wa kufikisha mawasiliano  vijijini kwa kampuni za simu Tanzania. Wanaoshuhudia (katikati) ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na  Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa. Hafla iliyoshirikisha makampuni ya simu, ilifanyika jijini Dar Es Salaam mapema wiki iliyopita. 


Wakuu wa kampuni za simu Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kusaini Mkataba wa Kufikisha Mawasiliano  Vijijini .

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga akizungumza na wageni waalikwakwenye hafla ya kusainiana mikataba na makampuni ya simu jijini Dar Es Salaam mapema wiki iliyopita. 


 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na  Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya kusainiana mikataba na makampuni ya simu jijini Dar Es Salaam mapema wiki iliyopita.

Loading...

No comments: