Vigogo 6 Jijini Mbeya Kortini kwa Kutafuna Bilioni 5 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, August 16, 2017

Vigogo 6 Jijini Mbeya Kortini kwa Kutafuna Bilioni 5

Aliyekuwa Mstahiki Meya Mbeya, Athanas Kapunga na wenzake watano akiwemo aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo Elizabeth Mnuo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Dkt Samwel Lazaro wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuingizia hasara serikali.

Viongozi hao ambao walishamaliza muda wao wamefikishwa mahakamani jana kwa kile kinachodaiwa kusababisha hasara kwa serikali ya zaidi ya bilioni 5.12 katika kipindi cha uongozi uongozi wao.

Watu wengine waliofikishwa mahakami ni aliyekuwa mweka hazina wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya James Jirojik, aliyewahi kuwa Mhasibu wa jiji hilo Tumaini Msigwa na Msimamizi mkuu wa Ujenzi wa Soko la Mwanjelwa Mhandisi Emily Maganga.
Loading...

No comments: