WADAU WAIOMBA TCRA KUBORESHA HUDUMA. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, August 3, 2017

WADAU WAIOMBA TCRA KUBORESHA HUDUMA.


                    Wanahabari wakisikiliza maelezo wa wataalamu kutoka Tcra hawapo pichani.

Na Sebastian Emmanuel jr,
Wakati mamlaka ya mawasiliano tanzania TCRA inapambana  kuboresha sekta ya mawasiliano hapa nchini wadau wameiomba mamlaka hiyo kutafuta muarobaini wa tatizo la wizi wa mitandao .

Rai hiyo imetolewa na waandishi wa habari wa mkoa wa Njombe katika semina iliyotolewa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kuhusu teknologia mpya ya kuhama mtandao bila kubadili namba ambapo wamesema kwamba kutokana na ukubwa wa tatizi la wizi wa mitandaoni ni vyema mamlaka ikaangalia jitihada za kukabiliana na tatizo hilo ambalo limewasababishiwa watumiaji wengi wa mitandao kuibiwa mamilioni ya pesa.
Kuhusu Teknologia hiyo mpya  wamesema inaweza kuwa na tija zaidi ikilinganishwa na ilivyokuwa awali kwani itawanufaisha watumiaji zaidi kutokana na ushindani utakaokuwepo baina ya makampuni ya simu.
Thadeo Lingo naibu mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA anasema ni wazi kwamba technologia ya mawasiliano ya simu imeleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali nchini na kwamba progaramu hiyo mpya ya kuhama mtandao bila kubadili laini itahimarisha zaidi usalama wa mtumiaji wa simu na kueleza kwamba hadi sasa watu zaidi ya mil 10 wameshafanikiwa kuingia kwenye programu hiyo mpya.
Akizungumza katika semina hiyo Bw Lingo amesema wameamua kukutana na waandishi  wa habari Mkoani hapa  kwani wanaamini kuwa elimu hiyo itasambaa mapema zaidi kupitia vyombo vyao vya habari.
Felisian Mwasigwa ni Mhandisi Mwandamizi wa Mawasiliano amesema kuwa mfumo huo utamsaidia mwananchi kuweza kutafuta mtandao ambao unaweza kumpa huduma ile anayoitaka na kusema kuwa huduma hii itaongeza ushindani katika makampuni ya mawasiliano.

Kwa  mujibu TCRA Tanzania inawatumiaji wa simu zaidi ya mil 40 na kudai hadi sasa tayari kuna watumiaji wa simu wasiyopungua mil 10 wamefanikiwa kujiunga na programu mpya ya kuhamia mtandao mpya bila ya kubadili laini.
Loading...

No comments: