Yaliyojiri kesi ya Manji Mahakamani kuhusu alivyopimwa mkojo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, August 23, 2017

Yaliyojiri kesi ya Manji Mahakamani kuhusu alivyopimwa mkojo

Kesi ya kutuhumiwa na matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji, leo imeanza kutolewa ushahidi wa vipimo vilivyochunguzwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali na majibu yake huku wakili wake akipinga kielelezo hicho cha mkojo hakikuwa halali.
Ushahidi umeanza kusikilizwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha shahidi wa kwanza alikuwa Ofisa Mkuu wa Makosa ya Jinai na Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam, Ramadhan Kindai na Askari Polisi Kitengo cha Upelelezi cha Makosa ya Jinai, Christopher.
Mahakamani hapo wakifafanua wameeleza hatua zote walizozifuata tangu Manji aliporipoti Kituo Kikuu cha Polisi, Februari 9 mwaka huu na kupelekwa kwa Mkemia kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo vya mkojo na hatimaye kugundulika anatumia madawa ya kulevya.
Wakili Hudson Ndusyepo ambae ni Wakili wa Manji aliukataa ushahidi wa barua iliyoandikwa ya Manji kupelekwa kwa Mkemia Mkuu ili kuchukuliwa vipimo vya mkojo kwa madai kuwa barua hiyo ilitakiwa kuwa na sahihi ya mteja wake kuridhia akachukuliwe vipimo hivyo.
Hakimu Cyprian Mkeha amehairisha kesi hadi Agosti 23,mwaka huu.


CHANZO; BONGO5
Loading...

No comments: