MwanaFA achekelea kutajwa na Fabolous kwenye party la ‘kinyamwezi’ - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, September 27, 2017

MwanaFA achekelea kutajwa na Fabolous kwenye party la ‘kinyamwezi’


Unanijua unanisikia ni moja  ya mistari  inayopatikana katika ngoma ‘Unanijua Unanisikia’ ya MwanaFA ambaye jina lake limetajwa na rapper Fabolous kutoka nchini Marekani,  aliyekuwepo katika party ya kinyamwezi na mastaa wakubwa duniani.
Party hiyo ilikuwa ni  ya uzinduzi wa bidhaa za BallyXSwizz kutoka kwa mtayarishaji wa muziki nchini Marekani, Swizz Beatz iliyokutanisha watu mbalimbali akiwemo mwanamitindo kutoka Tanzania, Flaviana Matata ambaye  ni rafiki wa Mwana FA na ndiye aliye rekodi video  ikimuonyesha ambayo Fabolous akimsalimia Mwanafalsafa(Mwana FA).
All my friends know how i ‘understand’ Loso..@flavianamatata done made my year,not a day not a week not a month,A YEAR aisee..thanks for the S/O @myfabolouslife i have always been a big fan! NB;Sjui kama ntawaruhusu kunywa hata maji siku mbili hizi,i cant promise 😜,” ameandika Mwana FA katika mtandao wake wa Instagram.
Kufuatia salamu hizo kunaashiria muziki wa Bongo Flava unakuwa kwa kasi hii ni baada ya mastaa kadha kuonyesha kuwatambua wasanii wa  Tanzania kama Diamond Platnumz, Alikiba ambaye ngoma yake ya ‘Seduce Me’ ilisikika katika sherehe hiyo na wengineo wengi na inatoa mwanya wao kufanya kazi katika nchi hiyo.
Loading...

No comments: