PILSNER KING YAZINDULIWA KWA AINA YAKE MWANZA


Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Limited ‘SBL’ imezindua kinywaji kipya ikiwa ni kuunga mkono Uchumi wa Viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye alihudhuria uzinduzi huo ameeleza kuwa kampuni ya SBL imesaidia kukuza uchumi wa Tanzania kwa kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja katika mifumo ya mauzo na usambazaji na vile vile hutoa ajira kwa wakulima nchini.
“Hii ni moja ya kampuni zinazotumia mazao yanayozalishwa nchini kwa kiasi kikubwa na hii inatusaidia kuwaelimisha wakulima kulima na kuzalisha mazao yenye ubora zaidi vilevile kwa mlengo wa biashara.” – John Mongella   


KWA HISANI YA MILLARD AYO.COM

Post a Comment

0 Comments