Viwanda vinavyotumia kuni kupigwa ‘stop’ December - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, September 26, 2017

Viwanda vinavyotumia kuni kupigwa ‘stop’ December


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba amebainsha kuwa viwanda vinavyotumia kuni mwisho wake utakuwa ni December mwaka huu.
Kauli ya waziri huyo imekuja mara baada ya kutembelea kiwanda cha chumvi Uvinza na kukuta kuni zikitumika kama nishati tegemezi. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter, Makanda ameandika;
Kiwanda cha Chumvi Uvinza hutumia kuni kukausha chumvi. Tumeamuru watumie jua. Wameanza. Wengine wote watumiao kuni viwandani mwisho Disemba.
Kufanikiwa kwa dhamira hiyo itakuwa ni mafanikio makubwa mengine kwa serikali dhidi ya kupigania mazingira ambapo mwanzoni mwaka huu ilitangaza kuwa mwisho wa pakiti za plastiki kufungashiwa pombe kali maarufu kwa jina la ‘viroba’ ingekuwa March Mosi na kweli wakafanikiwa kusimamia hilo hadi sasa.
Loading...

No comments: