Nyimbo za Bob Wine Zapigwa Marufuku - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, October 2, 2017

Nyimbo za Bob Wine Zapigwa Marufuku

Tume ya mawasiliano nchini Uganda (UCC) imepiga marufuku kwa vyombo vya habari nchini humo kufanya 'interview' na mwanamuziki Bobi Wine, baada ya kuonekana kinara kwenye suala la kupinga ukomo wa urais nchini humo. 
 
 
 
Taarifa hiyo imetolewa na mwenyewe Bobi Wine ambaye pia ni mbunge wa upinzani nchini humo kwenye ukurasa wake wa instagram akisema kuwa amepigiwa simu na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo na kuthibitisha suala hilo, kuwa wamepigwa marufuku kufanya naye mahojiano yoyote.
  
 
"Hii asubuhi nilitakiwa kufanya mahojiano na Capital FM, baadaye nikataarifiwa kuwa wamepewa agizo na UCC na kupigiwa simu na watu wa usalama kwamba wasiwe na mimi, nikapigiwa simu na vituo vingine vya redio na runinga na kunithibitishia wamepewa agizo hilo hilo na kwa vitisho, na iwapo watakuwa na mimi watakuwa katika hatari ya kufungiwa", ameandika Bobi Wine. 
  
 
Bobi Wine ameendelea kuandika akisema kwamba.. "Iwapo unaangalia dalili za kuanguka kwa serikali usiendelee tena, huu ni upumbavu na haukubaliki, serikali inadhani inaweza kutuzuia kufikia watu wetu, wanafanya vitu ambavyo havina tofauti na vile wanavyohubiri kuvipinga",
  
 
Bobi WIne amekuwa miongoni mwa viongozi maarufu ambao wanapinga vikali suala la kutaka kupitishwa kwa katiba ambayo itongeza muda wa ukomo wa urais, kitendo ambacho kitamruhusu Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo, kugombea tena awamu ijayo.
Loading...

No comments: