Askofu KKKT awaomba radhi waumini na maaskofu wenzake kwa kutousoma Waraka - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 30, 2018

Askofu KKKT awaomba radhi waumini na maaskofu wenzake kwa kutousoma Waraka


Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki, Dk Lucas Mbedule amewaomba radhi waumini wa dayosisi hiyo na Baraza la Maaskofu kwa kutokusoma waraka uliotolewa wa sikukuu ya Pasaka.

Askofu Mbedule ameomba radhi leo Aprili 29, 2018 wakati wa Ibada ya iliyofanyika kanisa la Mtwara Mjini, amesema licha ya salamu hizo kutokusomwa, anaunga nazo na yupo pamoja na maaskofu wenzake.

Akisoma barua ambayo ameituma kwa Mkuu wa KKKT, Askofu Dk Fredrick Shoo na maaskofu wote wa kanisa hilo, Askofu Mbedule amesema baraka za mababa maaskofu zilishindwa kusomwa kwa sababu zilizojitokeza wakati huo.

“Kwa njia ya barua hii, kwanza napenda kuwaombeni radhi kwa kuwakosesha baraka za mababa maaskofu,” amesema Askofu Mbedule.

Amesema yeye alishiriki kuuandaa na kutia saini na yupo pamoja na maaskofu wenzake.

Loading...

No comments: