#CHUKUAHII;Huyu ndiye mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi duniani kwa mwaka 2018 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 11, 2018

#CHUKUAHII;Huyu ndiye mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi duniani kwa mwaka 2018


Kama ulikuwa bado hujui mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi duniani kwa mwaka 2018, basi kitendawili cha jibu lako tayari kimeshateguliwa na kitabu maarufu duniani cha kutunza rekodi cha ‘Guinness World Records’ kimemtambua Mzee Masazo Nonaka kutoka Japan kuwa ndiye mwanaume mzee zaidi.

Oldest man certificate presentation
Masazo Nonaka akikabidhiwa cheti chake na Guinness World Records.
Kwa mujibu wa takwimu zilizofanywa na Kitabu hicho zimeonesha kuwa Mzee Nonaka mwenye umri wa miaka 112 ndiye mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi duniani kwa mwaka 2018.
Mzee Nonaka amezaliwa Julai 25, 1905 mjini Akoro nchini Japan na amefanikiwa kupata watoto watano na mkewe  Hatsuno Nonaka aliyefunga naye ndoa mwaka 1931 .
Nonaka amesema sababu kubwa iliyomfanya kufikisha umri huo ni kuoga maji ya uvuguvugu kila siku na kula vyakula vitamu.
Kwa upande mwingine, Mhariri Mkuu wa Kitabu cha Guinness, Craig Grenday amesema kuwa “tunayofuraha kumpata mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi duniani, Huu ni muda wa kujifunza vitu vingi kutoka kwa Nonaka namna ya kuifanya dunia kuwa na watu wengi wenye umri mkubwa”
Rekodi ya mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi duniani awali ilikuwa inashikiliwa na Muhispania  Francisco Nuñez Olivera aliyefariki mwezi Januari mwaka huu akiwa na miaka 113.
Hata hivyo, Rekodi ya mwanaume aliyeishi miaka mingi duniani inayoshikiliwa na Mfaransa aitwaye  Jeanne Louise Calment ambaye alifariki mwaka 1997 akiwa na miaka 122 .
Kitabu cha rekodi cha Guinness kimekiri wazi kuwa mpaka sasa bado hakijampata Mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani kwa mwaka 2018 ambapo rekodi hiyo bado inashikiliwa na Mjamaica, Violet Brown aliyefariki dunia mwaka 2017 akiwa na miaka 117 .

Loading...

No comments: