Hatua ya mazungumzo iliyofikiwa kati ya serikali na Acacia yaelezwa bungeni - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 11, 2018

Hatua ya mazungumzo iliyofikiwa kati ya serikali na Acacia yaelezwa bungeni

Serikali kupitia Naibu wa Madini, Stanslaus Nyongo imeeleza hatua ya mazungumzo iliyofikia kati ya Kampuni ya uchimbaji Madini ya Acacia na serikali.

Nyongo akiwa Bungeni mjini Dodoma leo, ameeleza kuwa serikali inaendelea na mazungumzo na uchunguzi uliotolewa maoni na zile Kamati mbili teule za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
“Ile taarifa ya Acacia ambayo walijicommit kutoa kishika uchumba serikali inaendelea na mazungumzo na uchunguzi uliotolewa maoni na zile Kamati mbili teule za Mh. Rais ni kwamba yale mashauriano yaliyotolewa na uchunguzi unaendelea na kama itaoneka katika vile vitofali kuna wizi wa dhahabu ulitokea kwasababu kulikuwa kuna under Decraration kama kweli ilitokea wao wa Acacia wako tayari kuweza kutoa au kulipa fidia zote ambazo wamejicommit na walitoa kishika uchumba cha dola Milioni 300,” amesema Nyongo. 
“Kwa maana kwamba walijicommit kwamba kama kutakuwa na pesa zingine za kutoa kwahiyo wataendelea kufidia kwamba maongezi yanaendelea na uchunguzi unaendelea na kama kuna upungufu wowote au kuna fedha yoyote inatakiwa ilipe katika halmashauri hela hiyo italetwa katika Halmashauri.”
Loading...

No comments: