#IdrisnaUber: Kampuni ya Uber imesaini mkataba na Msanii Idris Sultan kuwa Balozi wake nchini Tanzania mwaka 2018 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, April 21, 2018

#IdrisnaUber: Kampuni ya Uber imesaini mkataba na Msanii Idris Sultan kuwa Balozi wake nchini Tanzania mwaka 2018


Dar es Salaam, Tarehe 20 Aprili 2018.... Kampuni ya Uber imemtangaza msanii Idris Sultan kuwa balozi wake mpya nchini Tanzania mwaka 2018. Idris anakuwa msanii wa kwanza nchini Tanzania kuwa balozi wa Uber, programu ya usafiri yenye umaarufu mkubwa, nchini Tanzania.
Msanii huyu wa uchekeshaji, muigizaji wa tamthlia, na mtangazaji wa vipindi vya redio ametangazwa rasmi katika hafla ya kukata na shoka iliyokwenda kwa jina la #IdrisnaUber iliyohudhuriwa na wageni wachache na wanahabari wa humu inchini. Shughuli hiyo imefanyika katika mgahawa wa kifahari wa Akemi jijini Dar es Salaam.
Tangu mwanzoni mwa zoezi hili, tulifanya juhudi kubwa kuhakikisha kwamba tunampata balozi mwenye ufuasi mkubwa na atakayeiletea Uber ufanisi nchini Tanzania,amenukuliwa Bi.Elizabeth Njeri, Meneja wa Masoko wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki. Idris Sultan ni mcheshi na ni msanii ambaye hafanyi mambo yake kwa mazoea, pia anaheshimika katika tasnia ya uchekeshaji,tamthlia, na utangazaji wa vipindi vya redio. Tuna imani kwamba Idris atailetea Uber tija kubwa kwa sababu ni mzalendo kweli kweli - yeye ni kielelezo cha Utanzania na anawasiliana na mashabiki wake kupitia mitandao ya jamii kila wakati. Hizi ndizo sifa tunazosistiza tunapotaka kuwa na mkataba na mabalozi wa kampuni yetu kwa sababu zinasaidia sana katika kuonesha kwamba tunajali maslahi ya wasafiri na madereva wanaotumia mfumo wetu nchini Tanzania.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Bw Alfred Msemo; Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania, alisema; “Kampuni ya Uber inajituma kutumia uwezo wake kupitia oparesheni zake kimataifa ili kuwa karibu na wateja wake humu nchini. Mchango wa Idris Sultan katika muziki wa Tanzania unaendana na dhamira yetu ya kujenga kampuni ya kimataifa inayogusa maisha ya madereva na wasafiri wanaotumia mfumo wetu hapa nchini. Tutaendelea kuwahudumia wasafiri wetu sambamba na kutoa fursa za ajira kwa madereva wanaotumia mfumo wetu.
Idris alifurahi sana alipotangazwa kuwa Balozi wa Uber nchini Tanzania; “Nimefurahi sana na ni heshima kubwa kwangu kupata fursa hii adimu ya kushirikiana na Uber,kwa sababu mimi nishabiki mkubwa wa mapinduzi yaliyoletwa katika sekta ya usafiri kupitia kwa mfumo wake kote duniani. Nimefurahi kuona jinsi Uber imepata umaarufu jijini Dar es Salaam, binafsi mara nyingi mimi hutumia usafiri wa uberX nikiwa na marafiki zangu kwenye mitoko yetu ya jioni na sasa wamaleta huduma nyingine ya bajaji; uberPOA ambayo nina hamu sana kuitumia - utaniona hivi karibuni. Uber inaendelea kubadilisha maisha ya maelfu ya madereva jijini Dar es Salaam sambamba na kuwapa wasafiri uhuru wa kuchagua usafiri wanaotaka. Nimefurahi sana kuwa sehemu ya kampuni ambayo inajituma kuleta mabadiliko chanya katika maisha yetu.
Baadaye kwenye hafla hiyo, Idris alipanda jukwaani na kuwatumbuiza mashabiki, wanahabari,na wafanyakazi wa Uber kwa kionjo cha kazi yake ya uchekeshaji. Msanii huyo na mshindi wa zamani wa shindano la Big Brother Africa alivunja mbavu za umati huo kwa vichekesho vyake.  
Tangazo hili linakuja siku chache tangu Uber ilipo tangaza kushirikiana na Tigo kwenye mpango
ambao wateja wa Tigo wanapata bando za bure wanapotumia programu ya Uber. Ushirikiano
huu wa kipekee nchini Tanzania umekuwa na manufaa makubwa kwa wasafiri na madereva
wanaotumia Uber na umechochea wasafiri na madereva zaidi kujiandikisha kutumia programu
ya Uber nchini Tanzania.


Loading...

No comments: