Katibu Mkuu wa Fifa afikishwa kwenye kamati ya maadili

Fatma Samoura alijiunga na Fifa mwaka 2016 akitokea Umoja wa mataifaHaki miliki ya pichaAFP/GETTYS
Image captionFatma Samoura alijiunga na Fifa mwaka 2016 akitokea Umoja wa mataifa
Afisa wa juu wa Fifa, Fatma Samoura, amefikishwa mbele ya kamati ya maadili ya Fifa.
Samoura ambaye aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa chama hicho cha soka na Rais Gianni Infantino mwaka 2016, anatuhumiwa kukiuka maadili kwa kutoa siri za ndani huku pia akiwa na maslahi binafsi kinyume na taratibu za Fifa.
Hayo yametokana na shutuma kuhusu ombi la kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2026. Nchi hiyo inataka kuwa mwenyeji wa michuano hiyo lakini inapata upinzani mkali kutoka nchi za Amerika ya Kusini ikiwemo Canada, Marekani na Mexico.
Kikosi kazi cha kutathimini michuano hiyo, ambacho hivi karibuni kilitembelea nchi zilizoonyesha nia ya kuhodhi michuano hiyo, kimesema kimebaini kumekuwa na walakini kuhusu mahusiano kati ya Samoura ambaye jina lake kamili ni Fatma Samba Diouf na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, El Hadji Diouf, ambaye anafanya kazi ya ubalozi wa kuhakikisha Morocco inakuwa mwenyeji.
Samoura na Diouf ni raia wa Senegal, wote wanatuhumiwa kutokuwa na maadili juu ya suala hilo.
Afisa wa Fifa ameiambia BBC kuwa shutuma hizo hazina msingi, huku Samoura akisema kuwa alijua kua madai haya yatajitokeza na kwamba ''anajua ni nani anayetoa ujumbe huu''.
''nchi nzima ya Senegal itacheka kwa sababu kila mmoja nchini mwangu anafahamu mzizi wa El Hadji Diouf."
Hii ni mara ya tano kwa Morocco kuwania kuhodhi michuano ya kombe la dunia baada ya kuomba mwaka 1994, 1998, 2006 and 2010Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHii ni mara ya tano kwa Morocco kuwania kuhodhi michuano ya kombe la dunia baada ya kuomba mwaka 1994, 1998, 2006 and 2010
Afisa mmoja ambaye hakutaka kutambulika jina lake amemshutumu Infantino ''kuwahimiza'' kikosi kazi cha tathimini kutafuta ushahidi ambao utafanya Morocco kupoteza haki yake ya kuwania nafasi hiyo.
Akijibu shutuma hizo, msemaji wa Fifa ameiambia BBC kuwa " mchakato wa kumpata mwenyeji wa michuano ya 2026 unafuata sheria na uwazi na hivyo hakuna mtu anayepaswa kuwa na hofu juu ya hilo.
''Mchakato huu ni wa haki, hauegemei upande wowote na wa uwazi kabisa.''Ameeleza 
''Tathimini ya kikosi kazi inaongozwa na vigezo vilivyo wazi na visivyopendelea upande mmoja na ripoti yake itawekwa. 
Rais wa Fifa,Rais Gianni InfantinoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRais wa Fifa,Rais Gianni Infantino
Morocco ni taifa pekee la Afrika ambalo limeorodheshwa kati ya yale yaliyoomba kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia 2026 huku ikipata upinzani mkali kutoka kwa Canada, Marekani na Mexico ambazo zinataka kwa pamoja kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa duniani.
Mchakato wa kuwania kuhodhi michuano hiyo unakuja wakati Fifa ikikabiliwa na changamoto ya kifedha baada ya kuingia gharama kuwa kwenye maswala ya kisheria, kuhusu sakata la rushwa.Pia gharama za kuwavutia wadhamini kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi.
Inaaminika kuwa Infantino anataka Amerika ishinde kandarasi kwa kile kinachodaiwa kuwa itaingiza kiasi cha takriban dola za marekani bilioni 5 kutokana na shughuli za kiuchumi na dola bilioni 2.1 mapato ya tiketi pekee.

CHANZO; BBC SWAHILI

Post a Comment

0 Comments