Licha ya kudumu kwa miaka 6 kwenye uchumba, John Cena amwagana na mchumba wake - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 17, 2018

Licha ya kudumu kwa miaka 6 kwenye uchumba, John Cena amwagana na mchumba wake


Ikiwa ni mwaka mmoja tangu mchezaji maarufu wa mieleka, John Cena kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake waliyodumu naye kwa miaka sita kwenye mahusiano, Nikki Bella. Hatimaye wawili hao wametangaza kuvunja uchumba huo na kila mmoja kuishi kivyake.
Tokeo la picha la john cena Nikki bella
John Cena na Nikki Bella
Kwa mujibu wa mtandao wa US Weekly  umeripoti kuwa wawili hao wameachana na kufanya maamuzi hayo kuwa ya siri ili kuzingatia heshima ya kila mmoja.
Ingawaje maamuzi haya ni magumu lakini tutaendelea kuheshimiana na kupendana kama zamani. Tumejadiliana kwa kina juu ya tukio hili na tumekubaliana kulinda mambo yetu ya faragha hata baada ya kuachana kwetu,“wamesema wawili hao kwenye mahojiano yao na mtandao wa US Weekly.
Tetesi za wawili hao kuachana zilianza kusambaa mwezi uliopita lakini John Cena (40) alinukuliwa akisema kuwa hawaongozani pamoja kwa sababu ambazo alieleza kuwa angezitaja baadae.
Tujikumbushe tukio la John Cena alipomvisha pete mke wake Nikki Bella (32) ambaye naye ni mcheza mieleka mwaka jana Aprili 02.Loading...

No comments: