Mahakama Yatoa Amri Hans Pope Wa Simba Kukamatwa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 30, 2018

Mahakama Yatoa Amri Hans Pope Wa Simba Kukamatwa


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu imetoa amri ya Mwenyekiti wa Kamati ya  Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani hapo kuunganishwa katika kesi  ya utakatishaji fedha inayomkabili rais wa timu hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
  
Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha  kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani.
  
Amri hiyo imetolewa na hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya wakili  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini  (TAKUKURU), Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao.
  
Swai alidai kuwa  amewatafuta washitakiwa hao toka machi tatu mwaka huu  bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washitakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani.

Loading...

No comments: