Naibu Spika, Tulia Ackson Awatetea Mawaziri kwa Kumjibu CAG - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 16, 2018

Naibu Spika, Tulia Ackson Awatetea Mawaziri kwa Kumjibu CAG


 Naibu Spika, Tulia Ackson amewatetea mawaziri ambao wanashutumiwa kwa kutumia vyombo vya habari kujibu hoja za ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali wiki iliyopita.

Tangu Alhamisi ya wiki iliyopita, mawaziri wanne akiwamo wa Habari, Utamaduni na Michezo; waziri wa Fedha na Mipango na waziri wa Viwanda na Biashara walijumuika na kufanya mkutano na wanahabari wakijibu hoja za ripoti ya CAG.

Kitendo cha mawaziri hao kilikosolewa na wengi akiwamo Mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe.

Akizungumza bungeni leo Aprili 16, Dk Ackson amesema  mawaziri hao walikuwa wakitoa maoni yao kwa vyombo vya habari na si kujibu ripoti ya CAG.

“Kama ambavyo sheria isivyozuia CAG kuzungumza na vyombo vya habari, hivyo hivyo sheria haiwazuii mawaziri kutoa maoni yao kwa vyombo vya habari kuhusu ripoti ya CAG,” amesema Dk Ackson.

Hata hivyo amesema ni wajibu wa maofisa masuhuli kujibu ripoti ya CAG na kuwa hayo yanatakiwa kufanywa na mchakato wa Bunge.
Loading...

No comments: