Naiwaza Man United swala la uhamisho halipo akilini – Paul Pogba - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 24, 2018

Naiwaza Man United swala la uhamisho halipo akilini – Paul Pogba

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesisitiza kuwa mawazo yake yote yapo Manchester United kwa sasa na siyo uhamisho kama wengi wanavyotarajia.

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amewahi kusikika wakati wa derby yake na United akisema kuwa amewahi pata nafasi ya kuzungumza na wakala wa Pogba, Mino Raiola juu ya kumpatia ofa ya kiungo huyo kupitia dirisha la usajili la mwezi Januari.
Pogba amerejea kwenye fomu yake wiki za hivi karibuni baada ya kuishindia United ikitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 2 dhidi ya City  Aprili 7.
Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa amekiambia chombo cha habari cha  Canal Football Club, “Kwa sasa nipo Manchester United na ukweli ni kwamba nafikiria hapa nilipo kwa sasa, swala la uhamisho halipo kichwani mwangu. Tupo fainali yaya FA na kombe la dunia lipo karibu,”amesema Pogba.
Hata hivyo Poga amefanikiwa kuibuka nyota wa mchezo wakati wa nusu fainali  ya  FA dhidi ya  Tottenham kwa ushindi wa mabao 2 – 1 siku ya Jumamosi.

Loading...

No comments: