Rais Magufuli aitangaza Dodoma kuwa Jiji - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, April 26, 2018

Rais Magufuli aitangaza Dodoma kuwa Jiji


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameutangaza rasmi Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji kama ilivyokuwa baadhi ya mikoa ikiwemo Dar es Salaam.
Rais Magufuli amelitangaza hilo leo wakati wa sherehe za miaka 54 ya Muungano zinazofanyika kwenye uwanja wa Jamuhuri mkoani Dodoma.
“Kuanzia leo kwa mamlaka mliyonipa Dodoma ni jiji. Dodoma ni Jiji. Na Mkurugenzi wa hapa kuanzia leo anakuwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma,” amesema Rais Magufuli.
Wakati huo huo Mhe. Magufuli amesisitiza wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara kuulinda vizuri Muungano huo.
Loading...

No comments: