RASMI: Mfalme wa Swaziland, Mswati III abadilisha jina la nchi hiyo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, April 20, 2018

RASMI: Mfalme wa Swaziland, Mswati III abadilisha jina la nchi hiyo


Mfalme wa Swaziland, Mswati III ametangaza kubadilisha jina la nchi hiyo na kuanzia sasa itaitwa Kingdom of eSwatini kwa sababu alizoeleza kuwa jina la Swaziland ni jina lililoletwa na wakoloni kipindi nchi hiyo inapata uhuru mwaka 1968.
Picha inayohusiana
Mfalme Mswati III katikati kwenye picha.
Akihutubia maelfu ya wananchi Jumatano kwenye uwanja wa Somhlolo uliopo nje kidogo ya mji wa Mbabane katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo, Mswati III amesema jina la zamani la eSwatini lilikuwa na maana kuliko hili jipya la Swaziland na kutangaza nia ya kubadilisha jina hilo.
Mtandao wa Reuters umeripoti kuwa jana Alhamisi Aprili 19, 2018 kwenye sherehe yake ya kutimiza miaka 50 ya kuzaliwa iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Jubilee mjini Mbabane alitangaza rasmi kuwa nchi hiyo kwa sasa itaitwa Kingdom of eSwatini.
Akielezea sababu ya kufanya hivyo amesema anataka kuibrand nchi yake kwani anapokuwa kwenye mikutano ya kimataifa watu huwa wanachanganya majina kati ya nchi ya Switzerland ya Ulaya na jina la nchi yake Swaziland.
Hata hivyo, maamuzi hayo ya Mfalme Mswati III huenda alipanga muda mrefu kwani mwaka jana kwenye mkutano mkuu wa umoja wa mataifa mwaka 2017 alitumia jina la eSwatini badala ya Swaziland.
Jina la eSwatini kwa lugha ya kiswati lina maana ya ‘Ardhi ya Waswazi’.
Mfalme Mswati III ni mtoto wa amerithi cheo hicho kutoka kwa baba yake, Sobhuza II  mwaka 1986 na mpaka sasa anaripotiwa kuwa na wanawake 15.
Loading...

No comments: