Serikali kununua ndege kubwa ya masafa marefu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, April 26, 2018

Serikali kununua ndege kubwa ya masafa marefu


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali inatarajia kununua ndege nyingine kubwa ya saba ya masafa marefu na kueleza kuwa haitakodi kwa sababu kukodi ni gharama kubwa ikilinganishwa na kununua.
Prof. Mbarawa amesema Serikali haikurupuki kununua ndege hizo kwa kuwa inao mpango kazi unaobadilishwa kila mara kulingana na wakati.
Ameendelea kwa kueleza kuwa nia ya serikali ni nzuri kwani huwezi kuwa na viwanja vya ndege kama huna shirika lako la ndege, hivyo serikali imenunua ndege sita ambazo tatu zimetua na zinafanya kazi.
“Mwaka huu tunategemea ndege tatu zitawasilisha ambazo ni Boeng 787 ya masafa marefu yenye uwezo wa kuchukua abiria 262, nyingine mbili zenye uwezo wa kuchukua abiria 132 kila moja ni Bombardier CHCS 300 ambazo zitawasilia na kuanza kufanya kazi,” amesema.
“Kikawaida huwezi kuwa na ndege moja ya masafa marefu ikafanya kazi vizuri hivyo kwenye bajeti hii tumeshapanga kununua ndege nyingine boeng 787 ili tuwe na ndege mbili za masafa marefu ambapo moja ikiwa inatoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou na moja inatoka Guangzhou kuja Dar es Salaam. Ndio utaratibu unavyokwenda,” amesema.
Katika hatua nyingine ameongeza kuwa Kampuni ya Ndege (ATCL), inao mpango kazi hivyo si kweli kwamba haina kama wabunge walivyodai ambapo kila baada ya muda inabadilishwa kwani si msahafu hivyo itabadilishwa kutokana na mahitaji ya soko.

Loading...

No comments: