SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) LAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, April 29, 2018

SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) LAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa neno la utangulizi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu katika mkoa wa Simiyu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu katika mkoa wa Simiyu.kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw Festo Kiswaga .
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa( TANAPA) Allan Kjazi akikabidhi Hundi ya Kiasi cha Sh Mil 50 kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika mkoa huo ,wengine kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi ,Bw Festo  Kiswaga .
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ,Anthony Mtaka akiteta jambo na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za TAifa (TANAPA) Pascal Shelutete mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya makabidhiano ya hundi kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika mkoa wa Simiyu.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

Shirika la Hifadhi za Taifa leo limekabidhi mchango wa Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule tatu za vipaji maalumu katika mkoa wa Simiyu za Simiyu Ufundi , Simiyu Wavulana na Simiyu Wasichana .

Mchango huo umekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka.

Fedha hizi zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa shule maalum ya sekondari ya ufundi mkoani Simiyu ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya mkoa katika kuimarisha sekta ya elimu ambapo pia mkoa umepanga kuje nga shule nyingine maalum mbili za sekondari za  wasichana na wavulana.

 Kwa pamoja Mhe Mtaka aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga waliahidi kuzitumia fedha hizo kama zilivyokusudiwa na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umuhimu wa wananchi kuheshimu sekta ya uhifadhi kwa kuwa ina manufaa makubwa kwao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliahidi kuendelea kuwaunga mkono wana Simiyu kwa kuwa mkoa huo umekuwa mstari sa mbele katika kusimamia sheria za hifadhi hususan Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuzuia uingizaji wa mifugo pamoja na majangili.

Shule ya Ufundi ya Simiyu inatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 350 hadi itakapokamilika na wadau mbalimbali wameombwa kuunga mkono jitihada hizo za Simiyu.
Mwisho .
Loading...

No comments: