TANZIA: Mrembo Agness Gerald ‘Masogange’ afariki dunia - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, April 20, 2018

TANZIA: Mrembo Agness Gerald ‘Masogange’ afariki dunia

Video Queen maarufu nchini Tanzania, Agness Gerald maarufu kama Masogange amefariki dunia jioni ya leo Aprili 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, jijini Dar es salaam.

Agness Masogange enzi za uhai wake.
Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na ndugu wa karibu na marehemu, Dick Sound ambaye amesema mwili wa marehemu unasafirishwa jioni hii kwenda kuhifadhiwa mochwari- Muhimbili.
Wiki tatu zilizopita marehemu alishindwa kuhudhuria mahakamani kusikiliza kesi iliyokuwa ikimkabili kwa kulazwa hospitalini, hii ni kabla ya kesi hiyo kutolewa hukumu wiki iliyopita.
Mastaa mbalimbali wa muziki na waigizaji wa filamu wametoa pole kufuatia taarifa hizo za mshtuko za kifo hicho, na Bongo5 inatoa pole kwa familia yake katika kipindi hiki kigumu.
Taarifa zaidi juu ya msiba huo tutakuletea kaa nasi karibu.


CHANZO; BONGO5
Loading...

No comments: