Watumiaji wa WhatsApp wawezeshwa kurudisha picha walizofuta ndani ya siku 30


whatsappUlishawahi kufuta picha, video, waraka wa maandishi (document) au GIF kwa bahati mbaya katika WhatsApp yako? Na ukaanza kuhangaika kutafuta namna ya kurudisha na ikashindikana?
Kama ndio basi sasa WhatsApp wamekuja na suluhisho la kadhia hiyo. Baada ya watumiaji wengi wa WhatsApp kutaka kurudisha kile walichokifuta (picha au video) walizotumiwa bila kutumia programu maalum inawezekana!

Sasisho lijalo la WhatsApp litawawezesha watumiaji wake kurudisha mafaili ya picha za kawaida, za video, nyaraka na GIF ambazo zimefutwa mwezi mmoja uliopita (siku 30).

Kompyuta zenye uwezo wa hali ya juu (servers) za WhatsApp zitahifadhi data zako ulizofuta katika kipindi cha mwezi mmoja na ikiwa hutazirudisha katika kipindi hicho basi itakuwa ni vigumu sana kuvipata tena vitu hivyo bila kutumia programu wezeshi.

ndani ya siku 30
Hii itasaidia sana hususani pale mtumiaji atakapofuta aidha kwa bahati mbaya au kwa kukusudia na atakapogundua alichofuta ni muhimu na anakihitaji zaidi basi atakirudisha.
Lakini picha ambazo utaweza kuzirudisha ni zile za mtu aliyekutumia kama atakuwa hajazifuta kwa upande wako na iwapo amezifuta basi itabidi akutumie kwa mara nyingine tena. Kwa sasa unapofuta picha kwenye WhatsApp na kama hujafanya backup basi kuzipata picha zako inakua ni jambo gumu na linalohitaji ujuzi mkubwa wa kufanikiwa kurudisha.

Maboresho haya tayari yapo kwa majaribio kwa watumia wachache tu (wanaotumia WhatsApp BETA) na wale watakaopa sasisho 2.18.113 la WhatsApp ambao wanatumia simu za Android pekee. Kwa watumiaji wa iOS bado kuanza kupata kipengele hicho.

Post a Comment

0 Comments