WhatsApp yaboreshwa; Vitu vipya vya kuvutia vimewekwa


WhatsApp ambayo imezidi kuwa na watumiaji wengi kila kukicha kutokana na kile ambacho app hiyo imetengenezwa kurahisisha mawasiliano baina ya watu na watu au makundi iwe kwa mfumo wa video, ujumbe wa maneno au kupigiana simu.
Sio kitu cha ajabu kupata masasisho mara nyingi tu kutoka kwa wahusika (watengenezaji wa programu/app mbalimbali) na hii inatokana na kuona kuwa kuna umuhimu wa kuongeza kitu fulani kwenye programu ili kitu hicho kiweze kufanyika ambapo hapo awali kilikuwa hakiwezekani.

WhatsApp wameleta vipengele viwili vipya; kuweza kuzipa vipaombele taarifa fupi na kuweza kumtolea uwezo wa vitu anavyoweza kufanya kama kiongozi wa kundi.

  • Taarifa fupi zenye kipaombele.

Inawezekana kabisa wewe unafanya mawasilaino yako kwa asilimia kubwa kwa njia ya WhatsApp, iwe ni mambo ya kibiashara tu au masuala mengine tu hivyo kuwa jumbe nyingi kutoka kwa watu/makundi si kitu cha ajabu lakini mojawapo ya masasisho ya hivi karibuni ni kuweza kuweka kipaombele kwenye taarifa fupi (notifications) za kwenye WhatsApp. Kwa lugha rahisi ni kwamba zile taarifa ambazo utakuwa umezichagua ni za muhimu basi utaziona za kwanza kwenye orodha.
Vitu vipya vya kuvutia
Kwenye Settings>>Notifications ndio utaweza kuweka ili kuweza kuona taarifa fupi ambazo unataka kuziona za kwanza.
  • Kumuondolea mtu cheo cha “Kiongozi wa kundi” kwenye WhatsApp.

Hapa najua watu wengi watafurahia kipengele hiki 😀  😀 . Makundi ya kwenye WhatsApp yanaleta watu wengi sehemu moja na huenda wewe huna namba za watu wengi kuwaunganisha kwenye hilo kundi hivyo basi unampa mtu mwingine cheo cha kuwa kiongozi wa kundi hivyo kuweza kuongeza/kumtoa mtu kwenye kundi. Sasa vipi pale unaona mtu fulani hafai tena kuwa kiongozi wa kundi lenu kwenye WhatsApp?
Vitu vipya vya kuvutia
Unaweza kumuondolea cheo hicho bila ya hata kumtoa kwenye kundi.
Kipengele cha kumuondoleoa mtu cheo cha Kiongozi wa kundi kinapatikana kwenye Android, iOS na kwenye WhatsApp web toleo la 2.18.116. Kwa wale wanaotumia WhatsApp Tester (BETA) toleo la 2.18.117 watapata masasisho yote mawili.

Unazungumziaje masasisho hayo mawili ya kwenye WhatsApp?

Vyanzo: Gadgets 360, WABetaInfo

Post a Comment

0 Comments