Aliyemnunulia Zari gari na kutoswa, aibuka na mapya mazito - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, May 20, 2018

Aliyemnunulia Zari gari na kutoswa, aibuka na mapya mazito

Aliyemnunulia Zari gari na kutoswa, aibuka na mapya mazito

Baada ya Zari The Boss Lady kukataa gari aina ya Range Rover Sport ya mwaka 2017 kutoka kwa Ringtone Apoko ambaye ni msanii wa muziki wa Injili nchini Kenya, muimbaji huyo ameibuka na mapya tena.

Katika mahojiano na kipindi cha 10 Over 10 cha Citizen TV, Ringtone Apoko amesema kwa mara ya kwanza aliona taarifa za Zari kuachana na Diamond katika TV lakini kwake ilikuwa ni habari ya kawaida kama zilivyo nyingine.

Soma Pia: Msanii wa Kenya amnunulia Zari Range Rover Sport 2017, ni yule aliyetangaza kumuoa

Hata hivyo anaeleza kuwa alipokwenda kulala alijikuta akikosa usingizi kitu ambacho hakikuwa kawaida kwake.

“Kwa mapenzi ya Mungu kwa dakika chache nikapata usingizi, wakati nimelala nikaota na kuona Zari. Nikaamka nikasikia sauti ikiniambia Zari ndiye mtu sahihi kwangu,” amesema.

Soma Pia; Aliyetangaza kumnunulia Zari Range Rover Sport 2017 ala za uso

Wakati Zari akiwa nchini Kenya kwa ajili ya event yake ‘The Colour Purple’ iliyofanyika weekend iliyopita, alisema hamfahmu kijana huyo kwani ana watu zaidi ya milioni 3.9 katika mtandao wa Instagram ambao wanamfuatilia. 
Loading...

No comments: