Arjen Robben ajifunga mwaka mmoja Bayern Munich - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, May 12, 2018

Arjen Robben ajifunga mwaka mmoja Bayern Munich

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi, Arjen Robben amekubali mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kusalia ndani ya kikosi cha Mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani klabu ya Bayern Munich.

Robben mwenye umri wa miaka 34, ametua kwenye klabu ya Bayern inayoshiriki ligi ya Bundesliga akitokea Real Madrid mwaka 2009 na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya mwaka 2013.
Wakati huo huo beki wa Brazili, Rafinha amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja huku mkongwe mwengine wa Munich, Franck Ribery akiwa amesaini mkataba wa mwaka mmoja wiki iliyopita.
Loading...

No comments: