Bodi ya Ligi Yagoma Kuwakabidhi Simba Kombe Lao Singida - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, May 12, 2018

Bodi ya Ligi Yagoma Kuwakabidhi Simba Kombe Lao SingidaKikosi cha timu ya Simba SC.
BODI ya Ligi Tanzania (TPLB) imethibitisha kwamba Simba hawatakabidhiwa kombe lao leo Jumamosi lakini litakuwa jipya na ghali kuliko yale yaliyopita.
Simba ambayo imetawazwa mab­ingwa wapya tangu juzi Alhamisi, Yanga ilipopigwa mabao 2-0 na Prisons mjini Mbeya, leo itacheza na Singida United ugenini katika mch­ezo ambao Msimbazi walitaka ku­pewa ‘ndoo’ yao kabisa waiwahishe Bungeni jijini Dodoma Jumatatu.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura aliliambia Championi Jumamosi kuwa, kombe la Simba litakuwa jipya kwa sababu lile la awali, Yanga wamelichukua moja kwa moja ni sawa na kusema watapewa kombe moto.
“Kutokana na Yanga kuchukua ubingwa wa ligi mara tatu mfu­lulizo, kombe watakalopewa Simba litakuwa jipya,” alisema kiongozi huyo ambaye pia kitaaluma ni mwa­nahabari.
Habari za ndani ambazo Cham­pioni imezipata ni kwamba kombe hilo bado halijatengenezwa ndiyo maana Simba hawawezi kukabidhi­wa kwenye mchezo wa leo.
Habari zinasema kwamba vigogo wa Bodi ya Ligi wanakutana na wadhamini Jumatatu jijini Dar kujadili kuhusiana na muundo, aina na gharama za kombe hilo ambalo mashabiki wa Simba wanalisubiri kwa ‘mzuka’ mkubwa baada ya kulikosa kwa misimu mitano.
Lakini chanzo chetu kimetuthibi­tishia kwamba kombe la safari hii litakuwa ghali kuliko yale ambayo yamekuwa yakichukuliwa na Yanga misimu iliyopita na kwamba litakuwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 10 na litatengenezwa Dar.
Alisema kwamba, wanataka liwe la gharama kubwa kutokana na tha­mani ya ligi hiyo kupanda pamoja na uwekezaji ulivyo.
TFF imepanga kuiandalia Simba sherehe kubwa ya kuwakabidhi ub­ingwa wao katika mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumapili ya Mei 20, kwenye Uwanja wa Taifa ikiwa ni siku mbili kabla ya mchezo wa Yanga na Mbao.
Simba imeweka rekodi ya kuto­fungwa mpaka sasa katika mchezo wa 27 huku ofisa habari wake, Haji Manara, akiomba wapewe ‘ndoo’ yao leo.
Juzi baada ya Yanga kupokea kichapo, Manara alisema: “Tuna­waomba TFF, Bodi ya Ligi kwa ombi maalum watuletee uchampioni Singida, tumependa kombe letu tuk­abidhiwe huku kwa sababu tunataka kuwapa fursa wananchi wa mikoani na mikoa ya jirani wafurahie kombe na sisi mpaka tutakaporejea Dar.”
“Kuhusu shamrashamra za kurudi Dar na mapokezi tutawatangazia baadaye, kwa sasa tumepokea rasmi mwaliko wa kutembelea ofisi za bunge siku ya Jumatatu saa 4:00 asubuhi pale Dodoma.”
Wambura, alisema: “Kombe wa­tapewa kwenye mechi yao dhidi ya Kagera, kwa sababu kupewa kombe kuna shughuli mbalimbali zinafan­ywa, sio kombe linatolewa tu na kukabidhiwa, bali kuna vitu vingi vinaandamana na hiyo shughuli.
“Kumbuka haya matokeo ya ubingwa yamepatikana jana (juzi Alhamisi), sasa hizo shughuli mpaka uzikamilishe zote ili kuifanya hiyo shughuli ya kombe Jumamosi haitawezekana.
“Na sisi wala hawakutuandikia kwamba wanataka wakabidhiwe kombe na ni wajibu wetu kuwapa kombe baada ya msimamo kutuele­keza kwamba wanastahili kombe.”
Baada ya mchezo wa leo, Simba itasaliwa na michezo miwili dhidi Kagera utakaochezwa Dar es Sa­laam na itamalizia msimu mjini Songea kwa kucheza na Majimaji ambayo inang’ang’ania kubaki ligi kuu.
Loading...

No comments: