Conte Adai ana 'Uhusiano wa Kawaida' na Jose Mourinho - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, May 20, 2018

Conte Adai ana 'Uhusiano wa Kawaida' na Jose MourinhoMeneja wa Chelsea Antonio Conte amesema atamsalimia Jose Mourinho kwa mkono watakapokutana Chelsea wakikabiliana na Manchester United katika fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley Jumamosi.
Mameneja hao wawili wamekuwa na uhasama kila klabu zao zinapokabiliana Ligi ya Premia.

Lakini Ijumaa, Conte alisema: "Kesho, nitamsalimia kwa mkono na sote wawili tutafikiria kuhusu mechi."
"Si muhimu yale yaliyopita awali. Kuna uhusiano wa kawaida kati yangu naye."

Uhasama kati ya wawili hao ulianza Oktoba 2016, msimu wa kwanza wa Conte ligi kuu England pale Mwitaliano huyo alimpomshambulia Mourinho akisherehekea baada ya Chelsea kuwalaza United 4-0.
januari, Conte alimweleza Mreno huyo kama "mwanamume mdogo" baada ya kurushiana maneno kupitia vyombo vya habari.

Conte anatarajiwa na wengi kuondoka Chelsea majira ya joto na alipoulizwa kuhusu mustakabali wake, aliwachezea wanahabari na kusema: "Ninaweza kusema kwa kweli kwamba mechi hii itakuwa yangu ya mwisho, msimu huu.
"Kwangu na wachezaji, itakuwa mechi yetu ya mwisho. Kisha, kama mjuavyo vyema sana, nina mkataba na nimejitolea kwa klabu hii."

Mourinho alikataa kuzungumzia mustakabali wa Conte akisema: "Hadi iwe rasmi kwamba Antonio ameondoka, sijui. Kwa kweli, mkiniuliza kama nafuatilia hili - ni hamu tu ya kutaka kujua.
"Kuhusu mechi ya kesho (Jumamosi), iwapo itakuwa mechi yake ya mwisho au la, sifikiri hilo litabadilisha mtazamo wake kwa mechi hii na hamu yake ya kutaka kushinda."

Mourinho alipoulizwa kuhusu heshima kati yake na mashabiki wa Chelsea, alisema: "Kitu pekee ninaweza kusema kuhusu mashabiki wa Chelsea ni kwmaba tangu siku yangu ya kwanza 2004 hadi siku ya mwisho nilipofutwa miaka kadha iliyopita, waliniunga mkono kikamilifu," alisema Mourinho, 55, aliyeshinda vikombe vinane akiwa Stamford Bridge.
"Waliniunga mkono kila siku. Waliniunga mkono kila mechi, waliniunga mkono haa siku nilipofutwa - mara mbili, moja 2008 na miaka kadha iliyopita.

"Hilo sitalisahau kamwe kwa sababu walifanya kile ambacho ninaamini mashabiki wazuri hufanya, ambacho ni kumuunga mkono meneja wao hadi siku ya mwisho.
"Kuhusu mashabiki wa Chelsea, hilo sisahau: walikuwa wazuri sana."
Mourinho ndiye meneja aliyefanikiwa zaidi Chelsea baada ya kushinda mataji matatu vipindi viwili alivyokuwa Stamford Bridge mwaka 2005, 2006 na 2015.

Loading...

No comments: