Kaseja Atibua Sherehe Za Ubingwa Simba Mbele Ya Rais Magufuli - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, May 20, 2018

Kaseja Atibua Sherehe Za Ubingwa Simba Mbele Ya Rais Magufuli


Timu ya Simba imekubali  kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa leo Jumamosi.

Simba imekubali kupoteza mchezo huo muhimu ambao imetibua rekodi yao ya kutokufungwa mechi iliyoshuhudiwa na Rais John Magufuli.

Kagera Sugar imekuwa timu ya kwanza kuvunja rekodi ya Simba ya kutopoteza mchezo kwenye ligi msimu huu, ambapo mshambuliaji  Okwi alikosa penati  iliyopanguliwa na Juma Kaseja na kushindwa kuinusuru timu hiyo.

Simba imekabidhiwa kombe la ubingwa la Ligi Kuu msimu wa 2017/18 na Rais John Magufuli.

Loading...

No comments: