Kiongozi mbio za mwenge Agoma Kuzindua Mradi wa Milioni 500 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 9, 2018

Kiongozi mbio za mwenge Agoma Kuzindua Mradi wa Milioni 500


Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Charles Kabeho amegoma kuzindua mradi wa ujenzi wa nyumba tano za watumishi wa halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kwa madai kuwa thamani ya fedha za ujenzi zilizotumika haziendani na nyumba hizo.

Mbali na kukataa kuzindua nyumba hizo zenye thamani ya Sh511milioni, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mradi huo akibainisha kuwa kuna matumizi mabaya ya fedha za umma.

Tukio hilo limetokea leo Jumanne Mei 8, 2018 baada ya kiongozi huyo kutembelea mradi huo wakati mwenge wa Uhuru ukikimbizwa wilayani Kalambo mkoani hapa.

Kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi huo uliyotolewa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kalambo, Simon Kagani alieleza kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa Julai 2016 na kukamilika Aprili 2017 na kugharimu kiasi hicho cha fedha, ambapo Serikali Kuu imechangia Sh496milioni, halmashauri Sh15milioni.

“Siwezi kuzindua mradi huu kwa kuwa nimebaini thamani ya fedha haifanani na nyumba zilizojengwa. Milioni 500 kwa nyumba tano, ina maana kila nyumba ni Sh100milioni, sasa ndugu zangu kuna nyumba ya Sh100milioni hapa?” Amehoji.

Licha ya mkuu wa wilaya hiyo, Julieth Binyura na mwenyekiti wa halmashauri ya Kalambo, Daudi Sichone kutoa ufafanuzi wa ujenzi huo, hawakuweza kumshawishi kiongozi huyo wa mbio za mwenge.
Loading...

No comments: