Kiongozi mkubwa Korea Kaskazini amtukana Makamu wa Rais wa Marekani - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 25, 2018

Kiongozi mkubwa Korea Kaskazini amtukana Makamu wa Rais wa Marekani

Wakati dunia nzima ikisubiri kwa hamu mkutano wa kihistoria kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un na Rais wa Marekani, Donald Trump huenda mkutano huo usiwepo tena hii ni baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini kumtusi Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence.


Image result for Choe Son Hu
Choe Son Hui

Waziri huyo wa Korea Kaskazini, Choe Son Hui amemuita Pence kuwa ni Mjinga na Mpumbavu baada ya kauli yake aliyoitoa wiki iliyopita kuwa Korea Kaskazini ni sawa na Libya yote ni mataifa yaliyoanza pamoja kutengeneza vinu vya Nyuklia.
Kama mtu ambaye naifahamu vizuri Marekani, siwezi kushangaa kauli kama hizo za kijinga na za kipumbavu kutoka kinywani mwa Makamu wa Rais wa Marekani,“amesema kwenye mahojiano yake na shirika la habari la Korea Kaskazini la KCNA alipoulizwa kuhusu kauli ya Pence.
Hata hivyo, Bi. Hui amesema taifa lake huenda likafuta muda wowote mkutano kati ya Rais Trump na Kim Jong-Un  uliopangwa kufanyika June 12 mwaka huu nchini Singapore.
Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini wiki iliyopita alisema kuwa ili kudhoofisha au kuteketeza vinu vya Nyuklia katika mataifa yanayojihusisha na utengenezaji wa silaha hizo ni lazima utumiwe mfumo kama uliotumiwa Libya.
Je, kufuatia hali hiyo unadhani mkutano huo kati ya viongozi wakubwa wa mataifa hayo yenye nguvu kijeshi  unaweza kufanyika?
_______________________________________________________________________________________________
Loading...

No comments: