LHRC yakanusha taarifa ya kuteuliwa kwa Dkt. Kijo-Bisimba kuwa Mjumbe wa Baraza la wazee Chadema - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 31, 2018

LHRC yakanusha taarifa ya kuteuliwa kwa Dkt. Kijo-Bisimba kuwa Mjumbe wa Baraza la wazee Chadema


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), kimekanusha taarifa ya kuwa Bi Hellen Kijo Bisimba ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee Chadema. 
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)inaukumbusha umma wa watanzania kuwa Dkt. Helen Kijo-Bisimba bado ni Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC mpaka Juni 30, 2018.
LHRC kupitia ukurasa wake wa Twitter wameandika hivi: Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinakanusha taarifa hii na kuukumbusha umma wa watanzania kuwa Dkt. Helen Kijo-Bisimba bado ni Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC mpaka Juni 30, 2018.
Taarifa hii ni uzushi na ni ya kupuuzwa.
Taarifa iliyoelezwa ni ya kupuuzwa ni hii hapa chini:

Loading...

No comments: