MaDj wagoma kucheza ngoma za Kanye West nchini Marekani - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, May 7, 2018

MaDj wagoma kucheza ngoma za Kanye West nchini Marekani


Kauli ya Kanye West aliyoitoa wiki iliyopita kwenye mahojiano yake na mtandao wa TMZ akidai kuwa “Watu weusi walichagua kuishi kama watumwa kwa miaka 400“. Huenda ikawa imepokelewa kwa husuni na jamii ya watu weusi nchini Marekani kwani tayari MaDj wawili wa kituo maarufu cha radio cha 105.1 The Bounce mjini Detroit wamekataa kucheza ngoma zake kwenye kipindi chao.
Tokeo la picha la Kanye west
Kanye West
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Facebook wa kituo hicho cha Radio, MaDj hao maarufu mjini Detroit,  DJs BiGG na Shay Shay Say  wamesema kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya kuona kuwa maoni aliyotoa Kanye West kuwa watu weusi walichagua kuwa watuma yamefika mbali sana.
Imetosha kwa sasa, hatutaki tena kusikia wala kucheza nyimbo za Kanye kwenye kipindi chetu, hatutamzungumzia tena Kanye West. Kwa hili tunasimama wima kwa pamoja na hatutacheza nyimbo zake, tumekataa kumpa platform kabisa.“imeeleza taarifa yao waliyoitoa MaDJ hao.
We feel like Kanye has gone too far with his latest statement declaring that “slavery was a choice.” We are over it. We don’t want to hear Kanye’s music, we don’t want to play Kanye on our show, we don’t want to talk about Kanye anymore. So we are taking a stand and we aren’t playing his music anymore; we just are refusing to give him a platform. -BiGG & Shay Shay from the Morning Bounce #MuteKanye
Posted by 105.1 The Bounce on Thursday, May 3, 2018
Rapa Kanye West mnamo Mei 01, 2018 akiwa kwenye mahojiano na mtandao wa TMZ alinukuliwa akisema kuwa “Watu weusi walichagua kuwa watumwa kwa miaka 400” .
Hata hivyo, Kanye West bado ameendelea kutetea maoni yake kupitia ukurasa wake wa Twitter akidai kuwa alimaanisha kwa kizazi cha sasa cha jamii ya watu weusi kuishi na mawazo hayo ya kutawaliwa miaka ya nyuma ni utumwa pia.

Jiunge

Loading...

No comments: