Man United yaipiku Man City kwa kuingiza mkwanja mrefu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, May 12, 2018

Man United yaipiku Man City kwa kuingiza mkwanja mrefu


Licha ya kushindwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu, Manchester United imefanikiwa kuongoza kuingiza fedha nyingi za matangazo msimu huu.
Timu hiyo imeingiza kiasi cha paundi milioni 148.9 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 457 za Kitanzania kutokana na matangazo ya runinga kupitia BT Sport na Sky Sports.
Kupitia vituo hivyo Man United ilifanikiwa kuonyeshwa michezo yake 28 huku Manchester City na Arsenal michezo yao ikionyeshwa mara 25.
Man City wameingiza kiasi cha paundi milioni 147.4 wakifuatiw na Liverpool walioingiza kiasi cha paundi milioni 143.9.

Loading...

No comments: