Mlinga ampa kazi IGP kuhusu kina Mange - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 4, 2018

Mlinga ampa kazi IGP kuhusu kina Mange


Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kutumia nguvu alizonazo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwatukana viongozi huku akimtaja Mange Kimambi na wengineo kama vinara.


Akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya ndani kwa 2018/19, Mlinga amemtaka IGP kutumia nguvu alizowekewa mabegani kuwawajibisha watu wanaotukana kwani wamevuka mipaka hadi kufikia hatua ya Rais kutukanwa.

“Matusi mitandaoni ni 'too much', kwenye mitandao hajulikani Rais ni nani, kiongozi ni nani, kuna akaunti nyingi zinatukana, wanatukanwa wananchi, mawaziri mpaka Rais. IGP uko hapa tumekuwekea hizo nyota mabegani ni nguvu, tumia nguvu zako wasikuchezee. Mfano natoa akaunti zinazomtukana rais ni kama Kwinyara, Malisa GJ, Yericko Nyerere na Dada yao Mange Kimambi wamekuwa wakimtukana rais". Mlinga

Aidha Mbunge huyo ameongeza "Jamani hakuna nchi ambayo rais anachezewa. Mfano nimtolee mfano Kagame, umeshawahi kusikia mtu anamtukana Kagame? Polisi tumieni nguvu zenu". 
Loading...

No comments: