Mnyama ‘Simba SC’ hakamatiki VPL, Ndanda FC wafanyiwa kama Yanga - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, May 7, 2018

Mnyama ‘Simba SC’ hakamatiki VPL, Ndanda FC wafanyiwa kama Yanga


Klabu ya Simba imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara kwenye mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Emmanuel Okwi kulia kwenye picha
Goli pekee na la ushindi la Simba limefungwa na mshambuliaji wake Emmanuel Okwi kunako dakika ya 43 ya mchezo.
Matokeo mengine ya leo ni klabu ya Arsenal imekubali kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa Stand United,  magoli ya Stand yamefungwa na Sixtus Sabilo na Ally Ally huku la Azam likifungwa na Shaaban Idd.
Kwa matokeo hayo Simba kwa sasa wanakuwa na alama 65 wakifuatiwa na Azam FC wenye alama 49 na Yanga pointi 48.

No comments: