Picha: Belle 9 ajiandaa kuachia video ya ngoma yake mpya - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 25, 2018

Picha: Belle 9 ajiandaa kuachia video ya ngoma yake mpya

Ni miezi minne imepita tangu tuliposhuhudia video ya ngoma mpya ya Belle 9 ambayo inaitwa ‘Mfalme’ – Je unatamani kusikia ngoma mpya kutoka kwa msanii huyo?

Basi kuna uwezekano muda sio mrefu tukaona video ya ngoma mpya ya msanii huyo.
Wiki hii Belle ameonekana kupost picha takribani nne kwenye mtandao wake wa Instagram zikimuonyesha kama akiwa location kutengeneza kichupa hiko.
Lakini pia kunauwezekano wimbo huo ukapewa jina la ‘Dada’ kutokana na hashtag ambayo amekuwa akiitumia kwenye picha hizo huku akiandika baadhi ya maneno ambayo yanaonekana kuwa ni kama mashairi ya wimbo huo.
“Hufananii kuumia mapenzi mbegu ya mua na si rahisi kuyapata/,” ameandik Belle kwenye moja ya picha alizoziweka kwenye mtandao huo. Katika kuonyesha muda sio mrefu video hiyo itatoka, msanii huyo ameandika kwenye picha nyingine, “Maana ya mapenzi ni sisi tulivyo #DADA loading…..98%.”


Loading...

No comments: