PICHA: Spika Ndugai Alivyokaa Viti vya Wageni na Kutambulishwa Kama Mgeni

Leo Ijumaa Mei 25, 2018 Spika wa Bunge Job Ndugai aliketi  eneo maalumu kwa ajili ya wageni ndani ya ukumbi huo akiwa sambamba na mgeni wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.
Kikao cha Bunge kiliongozwa na mwenyekiti, Mussa Azzan Zungu ambaye alionyesha kushangazwa na kitendo hicho akidai ni jambo lisilo la kawaida.

Ndugai na mgeni wake walisimama kwa ajili ya utambulisho kama ilivyo kwa wageni wengine na kisha  kushangiliwa kwa nguvu na wabunge kabla ya kuondoka wakipitia mlango wa  wageni wa kawaida kisha wakazunguka kwenda ofisi ndogo ya Spika iliyopo nyuma ya ukumbi wa Bunge.
Tazama picha hapo chini 

Post a Comment

0 Comments