Q Chief asitisha mpango wa kuacha muziki ‘nimegundua mimi ni tatizo’


Muimbaji huyo kupitia mtandao huu alitangaza kuachana na muziki kwa madai anaona umemkataa kabisa na kila project aliyoitoa inashindwa kufanya vizuri huku wasanii wengine wanaofanya muziki unaofanana na wake wanafanya vizuri.
Akiwa katika kipindi cha XXL Cha Clouds FM Jumatano hii, Q Chief amedai baada ya kukaa na baadhi ya watu na kumshauri mambo mengi kuhusu muziki wake amegundua yeye mwenyewe ndiye mwenye tatizo na sio mtu mwingine.


“Kinachonitafuna mimi ni mimi mwenyewe, maisha yangu ya nyuma yananihukumu. Lakini I don’t want to be a prisoner of my past” alisema Q Chief.
Aliongeza, “Tangu nimetangaza kuacha muziki, nimeona mapenzi ya watanzania, nimeona mahaba yao, mpaka nimejiuliza tatizo sio support ya watanzania, labda ni mimi, au sikupata msaada niliohitaji ili kufanikisha maendeleo ya kazi yangu.”
Akiwa katika kipindi hicho, Q Chief alidai kati ya watu ambao aliwatafuta sana ili kupata msaada wakati muziki wake unaenda vibaya ni mtangazaji B Dozen lakini jitihada zake zikagonga ukuta. 


Katika kueleza hilo Dozen alisema. “Katika kipindi ulichonifuata nikusimamie sikuwa naweza kufanya hivyo. Ilifika kipindi wewe pia uliacha kunisukuma na unajua kuna majukumu mengi nafanya. Lakini hapa tuongee kitu cha maana ili kuendelea mbele. Mimi kama Dozen nakupa ahadi kama leo utasitisha uamuzi wako wa kuacha muziki, nakupa ahadi ya kukupa mchango wa mawazo, mbinu na kadri nitakavyojaaliwa ili kukusaidia kurudi unapostahili. Lakini siwezi kukuahidi kwamba tutatengeneza hits.”
.

KWA HISANI YA BONGO5.COM

Post a Comment

0 Comments