QNET inaleta Faraja kwa jamii zilizojiweza katika nchi 13 za kiafrika - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, May 21, 2018

QNET inaleta Faraja kwa jamii zilizojiweza katika nchi 13 za kiafrika

Mwakilishi wa kampuni ya QNET Tanzania  Andrew Gerald akikabidhi msaada wa vyakula wenye thamani ya 9mil/- kwa Mlezi wa kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasif  Dar Es Salaam,  Bi. Zainab Bakary kwa ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kampuni ya QNET inatoa msaada kwa nchi mbali mbali 13 barani  Afrika kwa ajili ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani.


Wawakilishi wa kampuni ya QNET Tanzania wakikabidhi msaada wa vyakula wenye thamani ya 9mil/- kwa Mlezi wa kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasif  Dar Es Salaam,  Bi. Zainab Bakary kwa ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kampuni ya QNET inatoa msaada kwa nchi mbali mbali 13 barani  Afrika kwa ajili ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani.


  • Kampuni hii inaleta tabasamu katika nyuso za kituo cha kulelea watoto cha Maunga Children Centre jijini Dar es salaam


Dar es Salaam, Mei 20 2018 - QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inayoongoza kwa kushirikiana na mwakilishi wake wa kijitegemea (IRs) kuleta shangwe na faraja kwa jamii mbalimbali zisizojiweza katika kuashiria mwezi mtukufu wa Ramadhan, katika nchi 13 za Kiafrika.

Kampeni hii ya mwaka ina lengo la kuboresha maisha ya wengi na inaenda sambamba na falsafa ya kampuni hii ya (RYTHM) Jiinue kuwasaidia wanadamu (Raise Yourself to Help Mankind) Mafunzo ya msingi ya (RYTHM) wakati wote yamekuwa yanalenga katika kuongeza juhudi zaidi ya wajibu katika  kujali wale ambao hawana uwezo kwa kuwapatia mazingira mazuri ya kuishi kwaajili yao, hasa watoto ambao ni alama ya kizazi chetu kijacho.  

Kampeni ya mwaka huu ya Ramadhan katika Afrika itashuhudia ushirikiano mkubwa miongoni mwa wafanyakazi wa QNET, wakala na Wawakilishi Binafsi (IR) wakiunganisha jitihada zao katika kuandaa mfululizo wa mwezi mzima wa shughuli za kutoa misaada katika nchi kama Ivory Coast, Togo, Cameroon, Guinea, Burkina Faso, Tanzania, Niger, Uganda, Chad, Mali, Ghana and Senegal.


Nchini Tanzania, tukio la utoaji wa misaada ya Ramadhan litashuhudia utoaji wa mchele, tambi, sukari na bidhaa zingine za chakula na matumizi kwa kituo cha Kulelea watoto yatima cha Maunga Children Centre jijini Dar es salaam.  

Kuna watoto 54 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Children Centre ambacho kilianzishwa katika mwaka 2008. Makazi haya ya watoto kwa sasa yanasimamiwa na Zainab Bakary na wanategemea misaada ya umma na wasamaria wema kuweza kukabiliana na gharama za mahitaji ya watoto ya vyakula na vinywaji.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo mwaka huu, Trevor Kuna, CEO wa QNET, amesema "Kampeni za kutoa misaada ya Ramadhan imekua moja kati ya kampeni zetu za msingi za kila mwaka.  Kwa kweli ni muhimu sana, inatia moyo na inakamilisha jitihada za QNET. Kampeni kama hizi huhamasisha uwezeshaji wa jamii na pia huwa zinahamasisha sana kwa wafanyakazi wetu na Wawakilishi wetu binafsi (IR's) kwa kushiriki wao binafsi katika kuboresha maisha ya engine.

Loading...

No comments: