Rais Magufuli ataka mikoa ya Njombe na Iringa kuchukua tahadhari dhidi ya Ukimwi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 3, 2018

Rais Magufuli ataka mikoa ya Njombe na Iringa kuchukua tahadhari dhidi ya Ukimwi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewahasa watu wa mikoa ya Njombe na Iringa kuchukua tahadhari juu ya gonjwa la Ukimwi kwasababu mikoa hiyo ndio inayoongoza nchini.

Akizungumza wilaya Kilolo mkoani Iringa katika uwanja wa Luganga, Leo Mei 2 wakati wa uwekaji wa Jiwe la msingi amesema kuwa Mkoa wa Iringa una 11.2% ya maambukizi ya VVU huku Njombe 11.6%.
“Mkoa wa Iringa na Njombe unamaambukizi mengi ya UKIMWI, Iringa una 11.2% na Njombe ni 11.6%. Inawezekana sababu ya msingi ni baridi lakini sina uhakika. Ni lazima tuwajibike katika kujikinga na UKIMWI,” amesisitiza Rais Magufuli.
“Kwahiyo Iringa ni ya pili Njombe ni ya kwanza kwa maambukizi ya Ukimwi nilipofika hapa Kilolo inaonekana shida kubwa hapa ni baridi na kwasababu inaletwa na Mwenyezi Mungu inabidi tujikinge na kuchukua tahadhari zote kwa gonjwa hili.” 
Hapo jana katika Siku ya Wafanyakazi(Mei Mosi) Rais Magufuli aliwaambia watu wa mikoa hiyo kuwa hali hiyo inatisha na anawomba kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo.

Loading...

No comments: