Rais Magufuli: Wafadhili wanne Wamejitokeza mradi wa reli ya kisasa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 3, 2018

Rais Magufuli: Wafadhili wanne Wamejitokeza mradi wa reli ya kisasa


Rais John Magufuli amesema zaidi ya wafadhili wanne wamejitokeza kutaka kufadhili mradi ujenzi wa reli ya kisasa baada ya Serikali kuanza mchakato huo peke yake.

Reli hiyo ya kisasa maarufu kama 'standard gauge' inajengwa kutoka Dar es Salaam, Morogoro hadi Dodoma.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Mei 2, 2018 wakati akizungumza na wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa mkoani Iringa.

Amesema fedha zilitokana na kuwabana mafisadi ambao hivi sasa wanamchukia kutokana na msimamo wake.

"Wameshatujua sisi ni wanaume ndiyo maana wamejitokeza kutaka kufadhili mradi huu ambao wakandarasi wameshapatikana na wapo eneo la kazi," amesema Rais Magufuli.

Loading...

No comments: