SABABU ZA ZIDANE KUJIUZULU MADRID - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 31, 2018

SABABU ZA ZIDANE KUJIUZULU MADRID

Zinedine Zidane ameushangaza ulimwengu wa soka baada ya kutangaza kujiuzulu kama kocha wa Real Madrid siku chache baada ya kushinda Ligi ya klabu bingwa  barani Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo.

Katika mkutano na waandishi wa habari  muda mfupi uliopita mapema leo, Kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 alithibitisha kuwa anajiuzulu baada ya ushindi wa Jumamosi 3-1 dhidi ya Liverpool huko Kiev.

Zizou alisisitiza kuwa "Madrid imenipa kila kitu na nitakuwa karibu na klabu hii kwa maisha yangu yote, lakini timu inahitaji njia nyingine na ndiyo sababu nimefanya uamuzi huu kwa ajili yangu na kwa kila mtu leo ​​kuna mabadiliko na ndiyo sababu nimefikia uamuzi huu.”


Zidane ameeleza kuwa kuwa kila kitu kinahitaji mabadiliko hivyo ni wakati wa mtu mwingine kuingoza klabu hiyo yenye historia kubwa katika nchi ya Spain.

Kocha huyo amefunguka kwa kusema kuwa amefarijika kuwa mmoja kati ya waliofanikisha Real Madrid kutwaa mataji 13 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuweza kuwa sehemu ya historia hiyo.

Kocha huyo amesema Real Madrid inahitaji kuendeleza rekodi yake ya kufanya vizuri haswa kuzidi kupata matokeo katika michuano mbalimbali mikubwa.

"Kitu ninachokiwaza ni timu iendelee kupata matokeo, inahitaji kuwa na mabadiliko na inahitaji mtu mwingine, naipenda Real Madrid" amesema Zidane. 

Zidane anaondoka Madrid akiweka historia ya kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya mara tatu mfululizo na kuweka historia kubwa ndani ya Santiago Bernabeu.

Loading...

No comments: