Salah atangazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka Uingereza


Mohamed Salah ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa Mwaka wa Uingereza kupitia tuzo za waandishi wa habari (FWA).
Salah tayari amepata tuzo ya mchezaji bora wa PFA na kutokana na kiwango chake, Liverpool ipo mbioni kumpa mkataba mpya na mnono kuepuka kuona yaliyotokea kwa Suarez na Coutinho.
Mo ameifungia Liverpool magoli 43 msimu huu kwenye mashindano yote msimu huu akiisaidia kuwa mguu mmoja tayari kwenye fainali ya klabu bingwa Ulaya na kuiweka katika nne bora EPL mpaka sasa.
Akiwa Chelsea pia alikabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wachezaji walioimarika na hakupata fursa za kutosha kuonyesha umahiri wake.
Raia huyo wa Misri alicheza mechi 19 kwa klabu hiyo ya London huku akianzishwa katika mechi tisa pekee. Ni mara mbili pekee alipocheza dakika zote 90. Salah baadaye alipelekwa kwa mkopo kwa vilabu vya Itali kabla ya kusainiwa na Roma kwa msimu wa 2015/16
Ni wakati huo ambapo Salah alionyesha umahiri wake na kufunga mabao 34 katika misimu miwili kabla ya kuelekea Liverpool.

Post a Comment

0 Comments