SBL kuendelea kufanya uwekezaji sekta ya viwanda

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akimkabidhi Tuzo ya Mshindi wa kwanza katika Makampuni matatu makubwa (TOP 3) Meneja wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Helene Weesie, wakati wa hafla ya Tuzo za 13 za Rais za Viwandani, (PMAYA) iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini DaresSalaam, mapema mwishoni wa wiki iliyopita .Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Charles Kimei.


Na Mwandishi Wetu
Viwanda, ni moja kati ya vichocheo muhimu kwa ukuwaji wa uchumi. Nchi zilizopiga hatua kubwa za kimaendeleo ikiwemo kwenye nyanja ya kiuchumi na ya kijamii, ni zile ambazo kwa kiasi kikubwa uchumi wake unaendeshwa na sekta ya viwanda.
Ni jambo lililowazi kuwa, nchi zenye sekta imara ya viwanda, zina uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi na pato lake ni kubwa ukilinganisha na zile zisizotegemea viwanda. Uchumi wa viwanda huongeza tija katika uzalishaji na kutengeneza ajira pia.
Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Novemba mwaka 2015, moja ya mambo iliyoyapa kipaumbele katika utekelezaji wa ahadi zake kwa watanzania ni kuifanya nchi kuwa ya viwanda.
Kupitia taasisi mbali mbali, serikali imekuwa ikihimiza ujenzi wa viwanda ikiwa ni pamoja na kutoa mazingira mazuri kwa viwanda vilivyopo na vinavyojengwa ili viweza kujiendesha kwa ufanisi na faida.
Siku chache zilizopita, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage alikuwa mgeni rasmi katika  katika utoaji wa tuzo za 13 za Rais za Viwanda (PMAYA) kwa mwaka 2017, ikiwa ni jitihada za kutambua mchango wa viwanda kwa uchumi wa nchi.
Akiongea katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, waziri Mwijage alisema, azma ya kukua kwa uchumi inategemea sekta ya viwanda na serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia 12 kwa mwaka, pato la taifa lisipungue chini ya asilimia 15 na ajira kuongezeka kwa asilimia 40 ya ajira zote
Mwijage alisema kuwa, serikali ya awamu ya tano toka iingie madarakan, imeweza kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwezesha kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
"Mpaka sasa toka Desemba 2015, tayari tumewahamasisha wawekezaji wa ndani na wa nje kujenga viwanda vipya 3,306 na tunawapongeza wawekezaji wa ndani na nje kwa kuchagua kuwekeza Tanzania na kuunga mkono serikali yetu ya kukuza uchumi wa viwanda kufikia 2025,” Mwijage.

Waziri Mwijage alisema zipo changamoto zinazotokana na wenye viwanda wenyewe ikiwemo udhaifu wa kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi ya Tanzania na kusababisha bidhaa za ndani kutokufahamika vizuti miongoni mwa watanzania na watuamiaji wa nje.Aliongeza sume kwamba kupitia baraza la Taifa la Uwekezaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), serikali itahakikisha watanzania wote wanashiriki katika ujenzi wa uchumi na kuongeza kuwa serikali kupitia baraza la uwezeshaji lina miradi ya kimkakati ya kusaidia viwanda vyetu na watanzania kwa ujumla kupata fursa mbalimbali zilizopo.

Katika hafla ya tuzo hizo zilizofana, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) iliibuka moja kati ya makampuni makubwa matatu yanayofanya vizuri kwenye matumizi ya nishati na kuweza kujinyakulia kikombe cha ushindi.

Akizungumzia ushindi wa kampuni yake, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie alisema,  kila mwaka SBL imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuhakikisha kuwa shughuli zake hazina athari kwa mazingira ikiwa  ni pamoja na matumizi sahihi ya nishati.

Mkurugenzi mtendaji huyo alisema, viwanda nya SBL vimekuwa vikitumia mkakati endelevu ya kutunza mazingira jambo ambalo limepelekea kupunguza matumizi ya maji na nishati katika uzalishaji wa bidhaa zake.

“Kupunguza matumizi ya nishati ni moja kati ya vipaumbele vikubwa katika shughuli zetu zote za kila siku.  Hii imetusaidia kupunguza upotevu usio wa lazima wa nishati, kutumia kwa usahihi vifaa vyetu na matumizi ya mashine zinazotumia nishati kidogo,” alisema Weesie.  

Weesie alisema, SBL inatekeleza mpango maalum ambao unawezesha kufuatilia, kupima na kuhakiki kiasi cha nishati kinachotumika katika kila mtambo na idara na kuongeza kuwa utaratibu huo hufanyika muda wote.

“Mpango huu unasaidia kugundua upotevu wowote wa nishati mara tu unapotokea na pia unahusisha wafanyakazi katika ngazi zote, aliongeza.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa, matumizi sahihi ya nishati ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kampuni hiyo na ukiachana na mitambo pia wafanyakazi wamekuwa wakisisitizwa kuokoa nishati kwa kuzima taa na viyoyozi (AC) wanapokuwa hawapo ofisini na hivyo kufanya suala la kubana matumizi ya nishati kuwa utamaduni wa kampuni

Akizungumzia mafanikio ya kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996 alisema, iliundwa na wajasiriamali wachache wa Kitanzania, SBL na kuanza na kiwanda kimoja kilichopo jijini Dar es Salaam amchacho kilikuwa kikizalisha bidhaa moja ambayo ni bia ya Serengeti Premium Lager na kuongeza kwa sasa kampuni inajivunia kuwa na bidhaa kadhaa zinazofanya vizuri sokoni.

“Bia ya Serengeti Premium Lager ilikuwa ndiyo ya kwanza kuzalishwa ikitengenezwa na kimea kwa silimia 100 huku ikifanikiwa kujipatia umaarufu mkubwa hapa Tanzania. Mwaka 2010 sehemu ya kampuni iliuzwa kwa kampuni ya kimataifa ya Diageo na kuwezesha kujengwa kwa viwanda vingine viwili Mwanza na Moshi,” alianikiza Weesie.

Weesie aliendelea kusema kuwa, hatua ya ujenzi wa viwanda hivyo vipya ulikwenda sambamba na kuongeza bidhaa ikiwamo bia ya Tusker, Pilsner pamoja na Guinness.

Akizungumzia mipango ya mbeleni ya kampuni hiyo alisema SBL itaendelea kupanua bishara yake na za washirika wake kwa  kusikiliza na kutekeleza matakwa ya wateja ambao ndiyo walaji wa bidhaa zao.

“SBL imekuwa ikisikiliza wanachokitaka wateja wake na kukitekeleza. Wateja wetu walituomba tuwatengenezee bia laini ya Kitanzania  na tuliwatengenezea bia Serengeti Lite ambayo imepokelea vizuri sokoni,” alisema.

Alisema kama mauzo yataendelea kukuwa kama ilivyo kwa mwaka huu, SBL itawekeza zaidi katika kipindi cha mwaka 1-2 ijayo jambo ambalo litazalisha ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na kupanua mpango wa kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji unaojulikana kama kilimo-biashara.

MWISHO…………

Post a Comment

0 Comments