Spika Ndugai aunga mkono usitishwaji wa kuweka mipaka (vigingi) - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 23, 2018

Spika Ndugai aunga mkono usitishwaji wa kuweka mipaka (vigingi)


Spika wa Bunge, Job Ndugai amekubaliana na ushauri wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wa kusitisha uwekaji wa mipaka (vigingi) katika mipaka ya hifadhi.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo jioni Mei 22, 2018 wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha vifungu vya bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2018/19.

Alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Serengeti (Chadema), Ryoba Chacha aliyebainisha kuwa uwekaji wa mipaka  haushirikishi wananchi.

“Ushauri uliotolewa na kamati naona ni mzuri tu, kabla ya kuweka vigingi mshauriane kwanza na kukubaliana. Lakini hili sijui la kuweka vigingi halafu baadaye uje usogeze sidhani kama ni sawa, Tanapa (Hifadhi za Taifa Tanzania) hili linawezekana kweli," amesema.

Baada ya kauli hiyo, wabunge walishangilia huku wale wa upinzani baadhi yao wakisimama kabisa kumuunga mkono.

Akihitimisha hoja yake, Chacha amesema: "Naungana na wewe mheshimiwa spika."

Loading...

No comments: